Wastara Aanza Matibabu Nchi India

Wastara Aanza Matibabu Nchi India
Msanii wa filamu za Bongo, Wastara Juma, tayari ameshawasili nchini India na kuanza rasmi matibabu ya mguu wake katika Hospitali ya Saifee nchini humo.

Wastara ambaye alichangiwa fedha na Watanzania mbalimbali walioguswa na hali yake hiyo ya kiafya akiwemo Rais John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli, aliondoka nchini juzi Jumapili, Feb. 4, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.

Msanii huyo maarufu amekuwa akisumbuliwa na mguu wake huo ambao ulipelekea kufanyiwa upasuaji na kupewa mguu wa bandia licha ya hali yake kubadiilika hivi karibuni na kudai kuwa amekuwa akipata maumivu makali ambapo baada ya kupata matibabu ya awalialishauriwa kwenda nchini India kwa matibabu zaidi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad