Watalii wa Kike Watakaojihusisha Kimapenzi na Wanaume Wazawa Kuchukuliwa Hatua

Watalii wa Kike Watakaojihusisha Kimapenzi na Wanaume Wazawa Kuchukuliwa HatuaMara nyingi imezoeleka kuwa mapenzi ni uhuru wa mtu binafsi na huwa haungiliwi na mtu mwingine labda iwe kwa ushauri tu lakini sio kwa jambo lingine. Kwa nchi nyingi za Afrika huwa watalii wanapofika kutoka nje imezoeleka kuona wakipata wachumba na wengine hata kuoana lakini hiyo ni tofauti kwa Gambia, ambako serikali imetangaza kuanza kuwachukulia hatua za kisheria watalii wa kike watakaojihusisha na mapenzi badala ya kitu kilichowaleta.
 Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Utalii nchini Gambia, Hamat Bah  juzi Februari 26, 2018 kwenye mahojiano yake na kituo cha runinga cha taifa hilo cha GRTS TV.

Hamat amesema kuwa kwa sasa ni msimu wa baridi barani Ulaya na watalii wengi kutoka barani Ulaya wanaongezeka kwa wingi nchini humo, na tayari kumekuwa na matatizo ya utapeli na kesi nyingi za baadhi ya watalii wa kike kuibiwa na wanaume wazawa.

Najua huu ni msimu wa baridi taifa linapokea watalii wengi kutoka Ulaya lakini tayari tumeanza kuwataarifu na kuweka machapisho mitandaoni kuwa watalii wa kike sana sana wasijihusishe na masuala ya mahusiano ya aina yoyote na wanaume wazawa isipokuwa wale wanaohusika kuwatembeza na kama itatokea basi mtalii huyo tutamrudisha upesi na kumchukulia hatua za kisheria mwanaume mzawa, kwani kesi za uporaji na udanganyifu kwa watalii wa wanawake zimekuwa zikiongezeka kila siku tunataka kukomesha tatizo hilo,“amesema Hamat.

Hata hivyo, Hamat amewataka watalii wa kike ambao wanaenda Gambia kwa ajili ya shughuli zozote za mapenzi iwe ni kujiuza au kutafuta wanaume wasiende nchini humo bali waende Thailand, ambako watakuwa huru kufanya hivyo la sivyo watakumbwa na mkono wa sheria.
Sisi sio kivutio cha mapenzi kwa watalii kuja kuzini, wanaotaka hivyo waende huko Thailand wakafanye hivyo. Tumekataa huo ujinga na kila Mgambia aimbe huo wimbo kuanzia leo, hatutaki kuipeleka hii nchi kwenye mazingira hayo, lazima nchi yetu tuilinde na kuitunza,“amesema Hamat.
Akizungumzia kuhusu matatizo mengine ya kiafya amesema kuwa wanaume wengi nchini Gambia, wanaamini kuwa watu kutoka barani Ulaya wana pesa na hawana maradhi, kitu ambacho
 kinasababisha kuongezeka kwa magonjwa ya ngono kama Ukimwi, kaswende n.k .

 Gambia hutembelewa na wastani wa watalii 200,000 kwa mwaka na wengiwao ni kutoka Uingereza, Uholanzi, na Marekani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad