Watendaji Wanaosimamia Zoezi la Vitambulisho vya Taifa Kuwa na Umakini na Uzalendo

Watendaji Wanaosimamia Zoezi la  Vitambulisho vya Taifa Kuwa na Umakini na Uzalendo
Serikali imewataka Watendaji wanaosimamia zoezi la usajili wananchi kwa ajili ya vitambulisho vya taifa kufanya kazi kwa umakini, uzalendo na kwa ushirikiano na jamii ili kuepuka kuandikisha na kuwapa watu wasio stahili vitambulisho vya raia.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.Mwigulu Nchemba wakati uzinduzi wa zoezi la usajili wananchi kwa ajili ya vitambulisho vya kitaifa mkoani humo.

Waziri huyo alisema kuwa miaka ya nyuma ambapo Watanzania walikuwa hawana vitambulisho vya Uraia, wapo wageni kutoka katika baadhi ya nchi waliweza kutumia mwanya huo kunufaika na huduma za jamii kama vile elimu ambazo zilipaswa kutolewa kwa Watanzania.

Alisema watu hao walipomaliza masomo walirudi kwao na kunufaisha nchi zao huku wakiwa wametumia pesa za Watanzania kujinufaisha wao na nchi zao na kusema zoezi hilo linahitaji umakini na uaminifu ili kubaini wageni na raia kwa ajili ya kuhakikisha kila kundi lisajiliwe kwa hadhi yake.

Dkt. Nchemba alisema kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake na kuhakikisha hakuna mgeni anayepenya kupewa Kitambulisho cha uraia kwa njia za udandanyifu.

Aidha Waziri huyo alisema zoezi la uandikishaji na utoaji wa vitambulisho hivyo ni bure , mwananchi hapaswi kulipa chochote wakati wa ufuatiliaji na kuongeza kuwa isitokee mtua akalipa pesa.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na vilevile watoto kuandikishwa shule ni lazima wawe na vyeti vya kuzaliwa na mitihani ya taifa form six usiandike bila kuwa na shahada ya uraia

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad