Watu Watatu Wakamatwa na Nyara za Serikali Zenye Thamani ya Milioni 33

Watu Watatu Wakamatwa na Nyara za Serikali Zenye Thamani ya Milioni 33
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, oparesheni na doria zenye tija ambapo February 5, 2018 katika maeneo ya Mwanjelwa Polisi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na nyara za Serikali ambazo ni vipande vinne vya meno ya Tembo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Mohammed Mpinga amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Kenedy Lupembe Simsokwe ambaye Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT – Tawi la Mbeya, Mathew Elikana Mwanjala ambaye ni Mpiga picha na Shaban Mkwiche.

Mpinga amesema baada ya kukamatwa na kupekuliwa, watuhumiwa walikutwa na nyara hizo ambazo ni Vipande vinne vya Meno ya Tembo ambavyo vina uzito wa Kilogram 5 na thamani yake ni Tshs 33,000,000/=. 

Kamanda Mpinga amesema taratibu za kisheria zinafanyika ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani na imeitaka jamii kuacha tabia ya kuwa na tamaa ya kujipatia utajiri wa haraka kwa kutumia njia za mkato zisizo halali, badala yake wafanye kazi halali ili kupata kipato halali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad