Watumiaji wa Mtando wa Snapcat Wataka Kubadilishiwa Mfumo

Watumiaji wa Mtando wa Snapcat Wataka Kubadilishiwa Mfumo
Moja kati ya habari za kimataifa leo February 15, 2018 ni kwamba siku chache baada ya mtandao wa Snapchat kubadili mfumo wake, watu Milioni 1 kutoka nchini mbalimbali Duniani wamesaini ombi la kuomba wamiliki wa mtandao huo kurudisha mfumo wa zamani wa kutumia mtandao huo.

Inaelezwa kuwa design hiyo mpya ya Snapchat ilifanyika kwa lengo la kutenganisha mwingiliano wa moja kwa moja baina ya marafiki na maudhui kutoka kwa watu maarufu na wenye ushawishi kwa namna tofauti.

Mwanzilishi wa Snapchat Evan Spiegel aliandika katika blog yake kuwa aliamini kuwa mwingiliano huo ulipelekea ongezeko la habari za uongo na ndio sababu za kuamua kubadilisha na kutenganisha maudhui hayo.

Watumiaji wa Snapchat wameeleza kuwa mfumo mpya huo wa mtandao huu ni mgumu kutumia ukilinganisha na uliopita na kwamba, vipengele vingi vilivyoongezwa kwenye mtandao huo havina maana na vinapoteza maana nzima ya kutumia mtandao huo tofauti na ilivyokuwa awali.

Kwenye mfumo huu mpya wa Snapchat, taarifa za marafiki wa mtumiaji zinaonekana na kupatikana upande wa kushoto wa ukurasa huo wa Snapchat huku taarifa za watu maarufu zinapatikana katika upande wa kulia tu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad