Waziri Nchemba afunguka kuhusu Akwilina


Dr Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro na timu ya uchunguzi kutoka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya kupigwa risasi kwa mwanafunzi Akwilina Maftah.

Waziri Nchemba ametoa maagizo hayo akiwa mkoani Geita wilaya ya Chato wakati wa uzinduzi wa Gereza la wilaya ya Chato.

Waziri Dr. Mwigulu amelitaka jeshi la polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kuchukua hatua kwa askari aliyehusika na hilo na kuwaambia wananchi nini kinachoendelea.

“Kama Waziri mwenye dhamana nalaani vikali sana tukio la kupoteza maisha ya binti wetu ambaye hakua na hatia, matukio ya namna hii naona yanaanza kujirudia tena kwa kasi matukio ya kupoteza maisha kwa watu wasiokuwa na hatia hasahasa katika masuala yanayohusu siasa ni mambo ambayo hayakubaliki na ninalaani kwa nguvu zote.” -Waziri Mwigulu

Dr. Mwigulu amewataka wananchi wote kuepuka vitendo hivi vinavyoweza kusababisha madhara kwa namna moja au nyingine na wanapoona matukio ya namna hii watoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili wahusika wafikishwe katika vyombo vya usalama.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mimi kwa maoni yangu naona polisi wasipokuwa makini wanaweza kujibambikia kesi isiokuwa yao. Kutokana na mazingira ya huyu mwanafunzi alivyouwawa ni lazima polisi wafanye uchunguzi wa kina kabla ya kukiri kuwa wao ndio waliorusha ile risasi iliompiga yule mwanafunzi. Inawezekana kabisa kukawa na mbinu chafu ya kulipaka matope jeshi la polisi na serikali. Vipi kwa mfano kama mulikuwepo watu pembeni wakisubiri ghasia zitokee ili wapate mwanya wa kufanya shambulio ili ionekane polisi ndio waliotenda? Polisi lazima wsichunguze risasi iliompotezea maisha yule Mwanafunzi kuwa ni ya kwao halisia la sivyo wahalifu wanaoweza kutumia udhaifu wa polisi kuwasukumia kesi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad