Yanga Yafunguka Kuhusu Mlinda Mlango Wao

Yanga Yakanusha Kuhusu Kusajiliwa kwa Mlinda Mlango Wao
Timu ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia Meneja wake Hafidh Saleh amefunguka na kudai si kweli jina la mlinda mlango namba moja wa timu hiyo, Youthe Rostand halijasajiliwa CAF kama baadhi ya watu wanavyodai.


Saleh ametoa kauli hiyo leo kupitia moja ya mtandao wa kijamii wa wanajangawani baada ya kuenea uvumbi wa muda mrefu kuwa mlinda mlango huyo hatoweza kucheza mashindano ya kimataifa kutokana na kutosajiliwa katikan Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

"Huo ni uzushi tu usiokuwa na maana, jina la golikipa Youthe Rostand limetumwa CAF na leseni yake ya kucheza mashindano ya kimataifa tunayo. Hivyo siyo kweli kwamba jina lake halikutumwa kama wanavyodai. Kuhusu kucheza au kutocheza mchezo inategemea na benchi la ufundi jinsi walivyopanga kulingana na mchezo husika", amesema Saleh.

Kwa upande mwingine, kikosi cha Yanga kipo katika mapumziko mafupi siku ya leo na kesho (Ijumaa) kikosi hicho kinatarajiwa kuendelea na mazoezi ikiwa ni matayarisho ya kuelekea katika mpambano wao wa marudio dhidi ya St Louis ya Shelisheli.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad