Yanga Yapewa Nafasi ya Kujiandaa Ligi ya Mabingwa Afrika

Yanga Yapewa Nafasi ya Kujiandaa Ligi ya Mabingwa Afrika

Mechi ya Yanga na Mtibwa iliyokuwa ipigwe hivi karibuni imeahirishwa ili kuipa nafasi Yanga kujiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ilikuwa na kibarua hicho cha kucheza na Mtibwa baada ya kukutana na Ndanda FC hata hivyo kwa mujibu wa mabadiliko hayo sasa mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine ili kuwapa nafasi wawakilishi hao kujiandaa vyema.
Yanga itakutana na Ndanda kesho Jumatatno kwenye mechi ya Ligi Kuu na baada ya hapo itapata muda wa kujiandaa mechi ya  Ligi ya Mabingwa Africa dhidi ya Township Rollers ya Botswana.
Mchezo huo dhidi ya Rollers ambayo wapo kileleni mwa Ligi Kuu ya Botswana ikiwa na pointi 45 msimu huu, utachezwa Machi 6, 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad