Arusha. Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ametaka uitishwe mkutano wa kitaifa wa maridhiano ili kujadili hali ya kisiasa na usalama nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Jana Jumamosi, Februari 24, 2018 jijini Arusha, Zitto amesema katika mkutano huo zijadiliwe changamoto zote za kisiasa na kukubaliana kanuni za demokrasia ya vyama vingi.
"Hii ni kutokana na dhahiri kuwa mfumo wa vyama vingi nchini upo hatarini zaidi kuliko wakati wowote,” amesema.
Amesema mkutano huo unatakiwa kuwashirikisha pia viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima na wafugaji.
Amebainisha kuwa hali ya kisiasa sasa si ya kuwaachia wanasiasa pekee kwa kuwa pia inahusu uhai wa watu na wengine ambao hata hawajihusishi na siasa.
Zitto yupo mkoani hapa kutembelea kata ambazo zina madiwani wa chama hicho na kuzungumza na wajumbe wa kamati za maendeleo za kata hizo.
Huyu Ni Zito au Titto?
ReplyDeleteKabla ya Zito Kabwe kudai kuitishwa mkutano wa kitaifa wa maridhiano ni vyema akawashauri wapinzani wenzake kutii na kuheshimu na kuitambua serikali iliopo madarakani kwani kama madai ni demokrasia basi demokrasia ya kweli ni kuheshimu maamuzi ya wengi na hapana shaka yeyote serikali iliopo madarakani Tanzania imewekwa na kukabalika na watanzania waliowengi. La kama Zito na washirika wake wanashaka na serikali iliopo madarakani kuwa sio maamuzi ya watanzania waliowengi basi kama kuna kipengele cha kuitisha uchaguzi mkuu wa dharura wa uraisi na wabunge basi wafanye hivyo ili kujiridhisha. CCM siyo wapumbavu kukubali kuyumbishwa na kikundi cha watu wachache wenye uchu wa madaraka kwa kisingizio cha kupigania demokrasia. Serikali iliopo madarakani ina sapota na watanzania wanaridhishwa na utendaji wake wa kazi kwa asilimia 90% na zaidi. Sasa maridhiano gani anayoyadai Zito na serikali? Zito kwa kujinasibu kuwa anavaa viatu vya Tundu Lisu na kwa Zito kujinasibu kuwa anavaa viatu vya Tundu Lisu inamaana yupo katika mkakati wa kuendeleza siasa za kiuharakati wa kuendeleza mapambano ya kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali iliopo madarakani na dhana ya kupinga na kubeza kila kitu kinachofanywa na serikali halali uliowekwa na wananchi waliowengi ni kitendo cha ughasi na uvunjifu mkubwa wa demokrasia. Zito anajulikana na harakati zake za kisaliti za kujikomba kwa mataifa ya kigeni kuhakikisha kuwa Tanzania inabanwa na jumuiya za kimataifa hasa katika masuala ya misaada na kadhalika. Kwa harakati zozote zile za Zito Kabwe na washirika wake wanazoziendeleza juu ya serikali halali iliopo madarakani iwe nje ya nchi au ndani ya nchi wajue bila shaka yeyote yakuwa mwishowe zinaishia ndani ya mikono ya serikali. Ila jumuiya za kimataifa sio wapuuzi wa kusikiliza kila upuuzi kwani wanaifahamu Africa na waafrica kuliko waafrica wanavyojifahamu. Na kwa upande wa jumuiya za kimataifa hakuna kitu kinachowakera zaidi kwa serikali za kiafrica kama corruptions. Ufisadi na vitendo vengine vya ubadhirifu kwa viongozi wa umma wa serikali za kiafrica ndio adui namba moja wa jumuiya za kimataifa. Ingekuwa rahisi sana kwa akina Zito na washirika wake kuitia misukosuko serikali ya Magufuli kwenye jumuiya za kimataifa kama madai yao yangelikuwa yanahusiana na masuala ya ufisadi. Na kwa upande mwengine wapinzani Tanzania wangekuwa na heshima zaidi duniani kama wangeliungana bega kwa bega na serikali ya Magufuli katika mapambano zidi ufisadi kuliko harakati ambazo wanazoziendeleza hivi sasa za kuitaka serikali iliopo madarakani kuwapigia magoti na kufuata matakwa yao, ambazo mimi naziona ni harakati za kijinga na zisizo na maono ya uweledi halisi wa siasa ya nchi na Dunia kwa ujumla kutoka kwa upinzani. Nchi kama Uganda. Rwanda. DRC CONCO. BURUNDI. Zitakupa picha halisi yakwamba kwa wapinzani wa siasa wa Africa kama wataamua kutumia nguvu kupambana na serikali zilizopo madarakani basi hakuna watakachofanikiwa isipokuwa ni kujitafutia mateso. Na kama Zito anaona harakati zao za kuifitinisha Tanzania na jumuiya za kimataifa zimefeli ni vyema kuwaomba radhi watanzania na serikali iliopo madarakani kwanza kabla ya kudai kuitishwa kwa mkutano wa maridhiano wa ktaifa kwani walisha tekeleza uharibifu wakutosha kwa taifa hasa katika suala la kuihujumu serikali iliopo madarakani ili ashindwe kuwatumikia watanzania katika kuwaletea watanzania maendeleo kikamilifu .
ReplyDelete