Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe jana usiku alikamatwa na kuchukuliwa maelezo katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro, ambapo baada ya maelezo hayo yaliyodumu kwa saa moja alipelekwa mahabusu kwa kunyimwa dhamana.
Polisi wanaituhumu ziara ya chama cha ACT Wazalendo kutembelea madiwani wao katika kata mbalimbali kwenye mikoa 8 nchini kuwa ni kosa kisheria.
Kwa mujibu wa maelezo ya Wakili wake, Mhe. Zitto ametuhumiwa kufanya Unlawful Assembly S. 74 cap 16 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Baada ya kuandika maelezo Zitto akiwa na Wakili wake, ndugu Emmanuel Lazarus Mvula, Maelezo ysliyoanza saa Saa 4:42 usiku wa jana, mpaka saa 5:40 usiku, Jeshi la Polisi limekataa kumpa dhamana na kumpeleka mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro.
Wakili Mvula amesema pia Jeshi la Polisi limekataa kusema kama dhamana ipo wazi au la, au kuweka wazi masharti ya dhamana.