Zuma Ahahirisha Hotuba ya Taifa

Zuma Ahahirisha Hotuba ya Taifa
Hotuba ya Rais Jacob Zuma iliyokuwa inategemewa sana bungeni Alhamisi wiki hii imeahirishwa, wakati shinikizo likizidi kuongezeka dhidi yake kuachia madaraka.

Spika wa bunge Beleka Mbete alitoa tangazo hilo bila kutoa tarehe mpya ya hotuba hiyo.

Baraza kuu lenye maaumizi makubwa ndani ya chama cha ANC wameitisha mkutano maalumu siku ya kesho, Jumatano.

ANC chazidisha shinikizo dhidi ya Zuma
Zuma akataa shinikizo la kujiuzulu
Bw Zuma amekataa kung'tuka sababu ya tuhuma za ufisadi.

Aliongoza mkutano na baraza la mawaziri leo asubuhi lakini uendelevu wa utawala wake haukuzungumzwa.

Vyama vya upinzani wanataka kura ya kutokuwa na imani naye ipigwe ilikutoa madarakani. Leo shirika la Nelson Mandela pia lilitoa wito ya kumuomba aachie kiti.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad