Afungwa Maisha Jela kwa Kubaka Mtoto

Afungwa Maisha Jela kwa Kubaka Mtoto
Moja ya stori ambayo ningependa ikufikie leo March 30, 2018 ni kumhusu Mwanaume aliefahamika kwa jina Shadrack Majimbo mwenye miaka 42 mkazi wa Nakuru Kenya, amehukumiwa kifungo cha maisha jela, kwa kumbaka binti wa miaka 9 na kumuambukiza magonjwa ya zinaa.

Hakimu wa Mahakama hiyo Judicaster Nthuku amesema ushahidi unaonyesha kuwa mtuhumiwa huyo alifanya vitendo hivyo vya ubakaji, ripoti ya daktari imethibitisha hilo huku akimuambukiza ugonjwa wa zinaa.

Imeelezwa kwamba mtuhumiwa alikuwa ni rafiki wa karibu wa familia ya binti huyo, ambapo siku ya tukio alimuita na kumtaka kumsaidia kazi za nyumbani, ndipo alipomfanyia kitendo hicho.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad