Baada ya Kichapo Toka kwa Township Rollers Yafunguka Kuhusu Mchezo wa Marudio

Baada ya Kichapo  Toka kwa Township Rollers Yafunguka Kuhusu Mchezo wa Marudio
Timu ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imefunguka na kudai itahakikisha mchezo wake wa marudiano dhidi ya Township Rollers inatoka na ushindi kwa kuwa wameshawajua wapinzani wao jinsi wanavyocheza hivyo haitawapa tabu.


Hayo yamewekwa wazi na Kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa baada ya timu yake siku ya jana (Machi 06, 2018) kuchapwa bao 2-1 katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya kufuzu makundi.

"Tumepoteza lakini hiki ni kipindi kimoja, nina imani kuwa mechi yamarudiano 'away' tutajitahidi kufanya vizuri ili tupate ushindi kama walivyofanya wao kwa kuwa tumewaona jinsi wanavyocheza. Kwa hiyo kikubwa tukiwa mazoezini tutajaribu kurekebisha makosa yetu tuliyokuwa tumefanya", amesema Nsajigwa.

Pamoja na hayo, Nsajingwa ameendelea kwa kusema "tulikuwa tunawaacha sana wakimiliki mpira wao kwa muda mrefu na kupelekea kushindwa kuwashambulia na pia tulikuwa kidogo tunachelewa kurudi nyuma ili kuweza kuwadhibiti wasiweze kufanya mashambulizi katika lango letu hicho ndio kikubwa nilichokiona. Tunajua tukienda kwao Botswana wanaweza kucheza mchezo tofauti lakini sisi tunajianda kwa jinsi tulivyokwisha kuwaona hapa nyumbani".

Mechi ya marudiano kati ya Yanga SC dhidi Township Rollers FC ya Botswana inatarajiwa kupigwa Machi 17, 2018 Jijini Gaborone Botswana ambapo Yanga italazimika kushinda zaidi ya mabao 2-0 ili kuweza kujihakikishia inatinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad