Kiungo mchezaji wa Simba, Jonas Mkude, aliumia jana wakati kikosi hicho kikijiandaa na mazoezi kuelekea mchezo ujao wa ligi dhidi ya Njombe.
Mkude aliumia wakati akiwania mpira na kiungo mshambuliaji, Mzamiru Yassin na kuepelekea kuanguka chini kisha kutolewa nje ya Uwanja wa Boko Vetarani.
Kufuatia kuumia huko, kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe, alisema Mkude hajapata maumivu makali, na anaweza akarejea baada ya siku mbili mpaka tatu.
Wakati Simba inajiandaa kuivaa Njombe Mji, Aprili 3 2018, kumekuwa na hofu kubwa kwa mashabiki kama ataweza kurejea mapema, japo majibu ya Daktrari yameeleza hatachukua muda mrefu.