Baba Daimond Aongea Mazito Sakata la Waziri Shonza na Daimond "Daimond Amefanya Makosa Kama Aliyowahi Kumfanyia Mimi"

Baba Daimond Aongea Mazito Sakata la Waziri Shonza na Daimond "Daimond Amefanya Makosa Kama Aliyowahi Kumfanyia Mimi"
SIKU chache baada ya staa ‘grade one’ wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kutoa maneno makali dhidi ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, baba wa msanii huyo, Abdul Juma ameibuka na kukumbushia ya nyuma (kufukua makaburi) kwa kusema amefanya makosa kama aliyowahi kumfanyia yeye!



Baba Diamond alisema amesikitishwa na kauli ya mwanaye dhidi ya Shonza.“Nimesikia yale mahojiano redioni yote na niseme kama mzazi sijapendezwa hata kidogo, kitendo chakumshambulia Shonza si kizuri hata kidogo na sijui kwa nini aliamua kutoa lugha kali kiasi kile,” alisema baba Diamond.



Baba Diamond alienda mbali zaidi kwa kusema kwamba, alichokifanya mwanaye ni muendelezo wa kileambacho aliwahi kumfanyia kipindi cha nyuma.“Tabia kama hii ya kutoa lugha ya dharau hajaianza jana wala leo, nakumbuka kabisa alishawahi kunifanyia kipindi cha nyuma hadi nikakata tamaa na kujihisi sina mtotokama unakumbuka ilifi kia kipindi nikasema hata nikifa asinizike, ameendeleza tabia hiyohiyo kwa waziri.”


Diamond.

“Haya na waziri Mwakyembe ameingilia kati na kusema hakufurahishwa na kitendo hicho, naungana naye kabisa si busara Diamond kushindana na serikali na kama ana ushauri basi autoe kistaarabu.“Kama mzazi amenikwaza sana na sijafurahishwa hata kidogo, ninachomuomba kwa sasa amfuate Shonza na amuombe msamaha,atambue yeye ni sehemu ya kioo kinachoangaliwa na jamii,” alimaliza baba Diamond.



Hivi karibuni, Diamond akifanyiwa mahojiano katika Kipindi cha The Playlist cha Radio Times FM kutokana na kufungiwa kwa nyimbo zake mbili; Waka Waka na Hallelujah, alitoa maneno makali akiwa na jazba dhidi ya Naibu Waziri Shonza kuwa hajawahi kusaidiwa na waziri huyo chochote kwenye muziki wake, anashangaa kumuona anakurupuka na kumfungia nyimbo zake.


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza.

Diamond alienda mbali zaidi na kusema kuwa, haogopi hata kwenda jela atakwenda ila ataitetea Bongo Fleva kwani anaijua kuliko anavyoijua waziri huyo na kwamba kitendo cha kumfungia nyimbo zake, hakukifanyia utafi ti kwanza.



Baada ya kauli hiyo, waziri Shonza alijibu amesikia malalamiko ya Diamond lakini hawezi kumjibu kwa sababu zipo taratibu za kufuata ikiwemo kuandika barua kama anaona hajatendewa haki Februari 28, mwaka huu, TCRA iliandika barua kwa vituo vya redio na runinga ikiviagiza visitishe kucheza nyimbo 15 za wasanii zikiwemo mbili za Diamond kutokana na kuwa na maudhui ambayo ni kinyume na maadili na kanuni za Huduma za Utangazaji(mwaka 2005).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad