Baby Madaha Ashindwa Kulipa Kodi Aamua Kuhamia kwa Shogaake

Baby Madaha Ashindwa Kulipa Kodi Aamua Kuhamia kwa Shogaake
SKENDO iliyomganda msanii wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ni ya kushindwa kulipa kodi kwenye nyumba aliyokuwa akiishi awali na kuhamia kwa ‘shogaake’ Issabela Mpanda ‘Bela Fasta’ maeneo ya Mbezi Beach.

Madai ya awali yalieleza kuwa, mambo sasa hivi yamemuendea kombo staa huyo kiasi cha mkwanja kumpitia pembeni, mazingira yaliyomfanya ashindwe kwenye baadhi ya mahitaji muhimu likiwemo hilo la kodi ya pango.

Kufuatia madai hayo, paparazi wetu alimtafuta Madaha na alipopatikana alishangazwa na madai hayo na kusema:

“Hayo ni maneno ya watu wenye chuki na mimi. Si kweli kwamba nimefulia. Na ifahamike kwamba siku nyingi nakuwa niko Dubai ambako nafanya shughuli zangu, ninapokuja huku Bongo kufikia kwa Bela siyo tatizo.

“Nilirudi hivi karibuni kwa ajili ya harusi ya mdogo wangu na siishi hapa kwa hiyo suala la kushindwa kulipa kodi na kwenda kuishi kwa Bela halina mashiko!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad