Kutokuwa na bajeti binafsi au ya familia imebainika ni chanzo cha mambo maovu katika jamii, maradhi ya akili na msongo wa mawazo kwa watu.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Iscot inayojihusisha na masuala ya ushauri wa mambo mbalimbali, Patrobas Mazara kwenye kongamano la kuwajengea uwezo wa matumizi ya fedha wafanyabiashara wanawake lililoandaliwa na Tanzania Women Chamber of Commerce. “Usipokuwa na utawala sahihi wa fedha yako unayoipata kama malipo ya shughuli unayofanya, utaishia kulalamika kila siku fedha haitoshi,” alisema Mazara.
Mmoja wa washiriki, Irene Kasubi alisema licha ya jitihada kubwa alizokuwa akizitumia kuhakikisha anafanikiwa alishindwa kufikka malengo.