Basata Wasema Diamond Amefanya Makosa Makubwa kumjibu Waziri Shonza

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza amesema mwanamuziki Nassib Abdul maarufu Diamond amefanya makosa kumjibu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akifananisha kitendo hicho na kuitukana Serikali.

Diamond Platnumz na naibu waziri huyo waliingia katika vita ya maneno baada ya Serikali kufungia nyimbo 15 mwezi uliopita, zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.

Mngereza amesema Diamond anapaswa kuelewa kwamba maneno machafu anayoyatoa dhidi ya waziri huyo  ni sawa na kuitusi serikali jambo ambalo hata ukienda katika sheria za kimtandao anaweza kujikuta anaingia matatizoni.

Mngereza amesema wamesikitishwa na kauli ya Diamond na kusisitiza kwamba ni vyema akafuata taratibu katika kulalamikia suala hilo ikiwemo kuandika barua kama alivyomuelekeza Waziri Shonza.

Ameongeza kuwa si lazima msanii aandikiwe barua pale anapokosa kama ambavyo Diamond ameeleza katika ukurasa wake wa Twitter, kwamba Shonza angemwandikia barua kabla ya kumfungia.

Amebainisha kuwa si kila mwanamuziki anayefanya makosa huwa anaandikiwa barua.

Katika malalamiko yake, Diamond amesema naibu waziri huyo amekuwa akikurupuka kufungia nyimbo na pia kutowaandikia barua rasmi ndio maana ameamua kuyazungumza kwenye redio na mitandao ya kijamii.

Jana Waziri Shonza alisema hawezi kujibizana na Diamond kwa sababu alichofanya si maamuzi yake binafsi na kwamba kama anaona ameonewa apeleke malalamiko yake kwa maandishi.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ili kupunguza ambiguous kati ya wasanii na wizara husika labda ingesaidia km taasisi husika 1)mfano,km ni swala la maadili ndo chanzo cha kutofautiana, inabidi Kwanza kulivunja-vunja neno hilo maadili kutoka kt hali yake ambayo ni more abstract na yenye uwezo mkubwa wa kusababisha ambiguities. Hizo ambiguities pengine ndo chanzo cha kazi za wasanii kufungwa, chanzo cha wasanii kufikiri wameonewa na ni chanzo cha wizara au taasisi husika kufikiri imefanya vema kuzifunga kazi za wasanii. Hivyo ni muhimu kulivunja-vunja neno maadili liwe kt indicators za wazi zaid kwa level ya understanding ya mtu yeyote. 2)itengenezwe policy ambayo ni very clear ikiliweka neno maadili lililovunjwa-vunjwa. Registered wasanii wote wapatiwe copies. Wasanii wapya wajuzwe na kusaini agreement before hand na taarifa km wanayo au hawana haki ya kupokea barua za warning iwe kwenye policy na wasanii walijue hilo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad