Bashe: Chochote Kitachonifika Amekipanga Kupeleka Hoja Binafsi ni Wajibu Wangu Kikatiba

Bashe Asimamia Msimamo Wake "Kupeleka hoja binafsi ni wajibu wangu kikatiba"
Mbunge wa Nzega Mjini (CCM),Hussein Bashe amesema amechukua hatua ya kuwasilisha hoja binafsi kwa Katibu wa Bunge kwa kuwa ni wajibu wake kikatiba.

Bashe amesema amechukua hatua hiyo kwa sababu amefanya uchunguzi kwa miezi mitano juu ya matukio ya utekaji, mauaji na watu kupotea yaliyotokea tangu mwaka 2010.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 8, 2018 huku akinukuu vifungu vya Katiba,  Bashe amesema hoja yake hiyo inawakilisha mawazo ya wananchi kuhusu matukio ya uhalifu, utekaji na watu kupokea.

Amesema katika hoja hiyo, ataambatanisha matukio ya tangu mwaka 2010 yakiwamo yaliyotokea katika uchaguzi mbalimbali kwa maelezo kuwa amefanya uchunguzi wa kutosha.

"Watanzania wanalalamika na haya ninayoyafanya yapo katika Katiba ya chama changu. Msingi wangu wa kubeba hii hoja ni katiba ya chama changu na katiba ya nchi.

"Ili CCM iendelee kuimarika lazima isimamie misingi yake. Nakwenda bungeni na hoja hii kama mbunge wa CCM. Nimechukua hatua hii sababu ni kiapo changu kwa Chama Cha Mapinduzi. Siwezi kulalamika mitaani nitatumia nafasi yangu kuwasilisha jambo hili," amesema.

Amesema mpaka sasa viongozi wa CCM waliouawa Kibiti wanafika 14, huku viongozi wengine wa upinzani nao wakipoteza maisha akiwamo aliyekuwa kiongozi wa Chadema, Alphonce Mawazo.

"Nani anafanya haya matukio mbona hakuna haki? Rais amezungumzia mambo haya likiwamo la Akwilina. Ila kauli ya Rais haizuii sisi wengine kufanya haya nifanyayo. Azory Gwanda mpaka leo hajulikani alipo," amesema.

Amesema kuwasilisha hoja hiyo ni kutimiza wajibu wake kama mbunge wa CCM,

"Nitaheshimu mawazo ya wengine kuhusu hoja yangu ili mwisho wa siku tufikie uamuzi kwa maslahi ya nchi na chama change,” amsema.

Amesema amefanya utafiti kwa zaidi ya miezi mitano na kwamba ataukabidhi utafiti huo ili kila Mtanzania ajue mambo hayo aliyoainisha katika hoja yake.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hayo matatizo ya kupotea au kuuwawa kwa watu yapo nchi zote Duniani na pengine Tanzania ndio nchi yenye matukio machache kabisa duniani na ndio maana imekuwa kama kitu kigeni yanapotokea. Lakini watu au watanzania wanatakiwa kutulia baadala ya kulichukulia hili suala kimihemko kwani ufumbuzi wake kamwe hauwezi kupatikana kutoka kwa hamasa ya mtu mmoja anaetaka kujifanya mjuaji wa kila kitu. Masuala ya ulinzi na usalama wa nchi yana watu wake ambao wapo qualified kuyashughikia vipi yeye Bashe anathubutu kusema kuwa amefanya uchunguzi wa zaidi ya miaka mitano, je yeye Bashe anataaluma yeyote kuhusiana na vitendo vya kihalifu? Na kama amefanya uchunguzi wa zaidi ya miaka mitano kutokana na matokeo anayodai yametokea kwanini asiwasiliane na kamati ya ulinzi na usalama ndani ya Chama chake au hata wahusika wakuu wa vyombo vya dola kwani yeye ni mwakilishi wa chama kinachoongoza nchi hii kitu gani kilichomfanya ashindwe kuwa na mawasilianao na taasisi husika zinazohusiana na masuala ya usalama ndani ya Chama na Serikali yake hata aamue kwenda kulipolitize suala nyeti kama la usalama wa nchi? Au kila mbunge CCM anafanya kazi kivyake hakuna kitu kama hicho ndani ya CCM yaani kama chama tawala masuala yanayoyahusu serikali ni ya Chama pia lazima kuwe na coordination miongoni mwa watendaji wake kabla ya mambo kutoka nje? Lakaini Kwa vyovyote vile harakati za Bashe ni za kisiasa zaidi na zinazoweza kuleta taharuki zaidi katika jamii zilizojikita katika kujijengea sifa binafsi kuliko ufumbuzi wa tatizo. CCM Wakati mwengine lazima watambue yakuwa, An honest enemy is better than a false friend.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad