Bocco Awaomba Mashabiki wa Simba

Bocco Awaomba Mashabiki wa Simba
Nahodha wa klabu ya soka ya Simba mshambuliaji John Bocco, amewaomba mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mechi ya kesho dhidi ya Al Masry kwani ni nafasi nzuri ya timu yao kuwapatia furaha.


''Kesho tunaimani tutacheza mchezo mzuri na tutawapa raha mashabiki wetu, ukizingatia mechi iliyopita dhidi ya Stand United hatukupata matokeo mazuri hivyo kesho ni nafasi nzuri ya kuwapa raha Wanasimba'', amesema Bocco kwenye mkutano na wanahabari.

Simba kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa kwanza wa Kombe la shirikisho Barani Afrika dhidi ya Al Masry kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kuanzia saa 12:00 jioni.

Kwa upande mwingine Bocco amesema wamejipanga kucheza kitimu zaidi kesho ili kuepuka makosa ya mtu mmoja mmoja ambayo yamekuwa yakiigharimu timu katika mechi za hivi karibuni.

Kikosi cha Al Masry ambayo inashika nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 48 kwenye mechi 25 ilizocheza tayari kipo nchini tangu jumamosi iliyopita.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad