''Bongo Movie Mnapaswa Kuwa na Nidhamu'' Joyce

Wasanii wa Filamu nchini wametakiwa kuwa na nidhamu ili kuwasaidia kuaminika kwa jamii kitu ambacho kitarahisisha ufanyaji wa kazi zao kutokana na taasisi za kifedha kuwasaidia.

Rai hiyo imetolea na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) Joyce Fissoo, alipokuwa akiwasilisha mada katika kikao kazi cha maafisa Utamaduni na wadau wa filamu kilichofanyika mkoani Arusha.

”Mnapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, wasanii wengi hasa wa tasnia ya filamu mmeshindwa kuaminiwa kutokana na nidhamu inayotiliwa mashaka na wadau wenu ambao mngeweza kufanya nao kazi” amesema Mama Fissoo.

Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Hargeney Chitukuro ameishukuru Bodi ya Filamu kwa kuupa mkoa wao fursa ya kukutanisha wadau wa tasnia hiyo na wao kama Serikali ya Mkoa wako tayari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha vijana wanapata ajira ya uhakika kupitia filamu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad