CAG Aomba Radhi Wananchi Juu ya Taarifa ya Deni la Taifa Aliyompa Rais Magufuli "Yalikuwa Makosa ya Kimatamshi Deni ni Himilivu"

CAG Aomba Radhi Wananchi Juu ya Taarifa ya Deni la Taifa Aliyompa Rais Magufuli  "Yalikuwa Makosa ya Kimatamshi Deni ni Himilivu"
Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Profesa. Mussa Assad ameomba radhi wananchi na serikali juu ya taarifa ya deni la taifa na kusema kuwa yalifanyika makosa ya kimatamshi deni hilo ni himilivu.


Profesa Assad ametoa taarifa hiyo mjini Dodoma ambapo amesema deni halisi ni shilingi trillion 46.08 na ni himilivu hivyo anaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa wananchi na taasisi za serikali.

"CAG anapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kauli yake aliyotoa kuhusiana na mwenendo wa na ukuaji wa deni la taifa kama alivyonukuliwa wakati akitoa ripoti hizo kwa Mhe. Rais Magufuli taarifa sahihi kuhusu mwenendo wa deni ni kwamba kwa kujibu wa taarifa ya maandishi wa CAG hadi kufikia tarehe 30 Juni 2017 deni la taifa lilikuwa ni trilioni 46.08 katika deni hilo deni la ndani ya trilioni 13.34 sawa na asilimia 16 na deni la nje nu trilioni 37.75 ambayo ni sawa na asilima 71, kwa hivyo utafiti umebaini kuwa deni la taifa kwa sasa ni himilivu"

CAG wakati akitoa ripoti hiyo kwa Rais John Pombe Magufuli kuhusu suala la muenendo wa deni la taifa alidai kuwa deni la taifa si himilivu lakini kwa mujibu wa utafiti ambao wamefanya wao CAG ameibuka na kuomba radhi na kusisitiza kuwa ripoti ya CAG ni siri hadi itakapowasilishwa bungeni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad