Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe MDC kimewafukuza maafisa wake watatu wa juu kutokana na kuwa na tabia zisizokuwa za kikatiba.
Kati ya waliofukuzwa ni naibu waziri wa chama hicho,hatua ambayo inakidhoofisha chama miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu.
Chama cha MDC kitachuana na rais Emmerson Mnangagwa aliyechukua nafasi ya Robert Mugabe mwezi Novemba,katika uchaguzi wa urais mwezi Julai.
Kiongozi na mwanzilishi wa chama hicho Morgan Tsvangirai alifariki mwezi Februari baada ya kuugua ugonjwa wa saratani.
The opposition has picked 40-year-old Nelson Chamisa as its leader and presidential candidate, but some senior party officials have accused him of a power grab.
Upinzani umemchagua Nelson Chamisa mwenye umri wa miaka 40 kama kiongozi wake lakini baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wa chama hicho wamemshutumu kunyanyakua madaraka.