Darassa Apotezwa na Dawa za kulevya ?


Darassa Apotezwa na Dawa za kulevya ?
Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, Abba amefunguka na kudai si kweli ukimya wa Darassa unatokana na matumizi ya dawa za kulevya kama baadhi ya watu wanavyodhani na kuwataka wawe wavumilivu kwani muhusika mwenyewe atakuja kujitokeza.
Abba ametoa kauli alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz inayorushwa na EATV baada ya kuonea mfululizo wa tetesi zinazomuhusisha Darasa na matumizi ya dawa za kulevya na kupelekea kupotea katika tasnia ya muziki mpaka hii leo.

"Nashindwa kuwaelewa kwa jinsi mnavyosema Darasa haonekani sasa mmemuona vipi akiwa anatumia dawa za kulevya ?. Darasa yupo poa kabisa na labda hayo madude wanaosema wao wanayatumia wenyewe kwenye ndoto zao wanaoziota hao watu", amesema Abba.
Pamoja na hayo, Abba ameendelea kwa kusema "Darasa yupo poa na familia yake na wala hatumi kitu chochote mimi kama mwanae nasema yupo 'fresh' na kila siku nipo na Darasa na muda wote nikimuhitaji huwa nampata".
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Siku zote zile uongo miguu yake ni mifupi sana na kifanyikacho gizani ipo siku kitaonekana kwenye muangaza ili wenye macho wakione so it's a matter of the time only

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad