Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema deni la Taifa linatia wasiwasi hivyo Serikali inatakiwa kuchukua hatua kupunguza ukubwa wa deni hilo.
Profesa Assad ametoa kauli hiyo leo Jumanne Machi 27, 2018 na kubainisha kuwa deni hilo ni Sh46 trilioni kutoka Sh41 trilioni la mwaka uliopita, kwamba ni ongezeko la asilimia 12.
Ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa uwasilishaji wa ripoti yake ya ukaguzi mwaka 2016/17 iliyobaini madudu Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma.
“Tulichosema hapa kwa kweli ukuaji wa deni tunasema ni himilivu lakini jinsi linavyoongezeka tunakaribia maeneo ya wasiwasi. Asilimia 72 ya GDP (Pato la Taifa) siyo mbaya lakini ikifika asilimia 76 nchi nyingine zimepata shida, inabidi tuangalie sasa namna gani tunaweza ku-control ukuaji wa deni hilo,” amesema.