Diamond Aiponza Times FM, TCRA Yawawataka Kuwasilisha Kipindi Chote Walichofanya Naye Mahojiano

Diamond Aiponza Times FM, TCRA Yawawataka Kuwasilisha Kipindi Chote Walichofanya Naye Mahojiano
Kituo cha Redio Times cha jijini Dar es Salaam kimetakiwa kuwasilisha kipindi cha mahojiano waliyofanya na mwanamuziki Diamond Platinumz kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mkurugenzi wa Times FM, Amani Misana ameieleza MCL Digital leo Machi 22, 2018 kuwa amepokea barua ya kuwataka wawasilishe kipindi hicho kilichorushwa Machi, 19, 2018 na kwamba leo wametekeleza agizo hilo.

“Tumepokea barua na tumefanya yale tuliyoagizwa ikiwamo kuwasilisha kipindi chote,” amesema kwa ufupi Misana.

Kaimu Meneja Mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakyanjala amesema suala la kituo hicho kupewa barua ni la kiutawala zaidi na mamlaka hiyo haipo kwenye kitengo chake isipokuwa kama tayari barua imefika, wakati wa kutolewa uamuzi vyombo vya habari vitaalikwa.

Mwanamuziki Diamond alizua mjadala baada ya kuzungumzia suala la nyimbo za wasanii kufungiwa akimlalamikia Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kutowatendea haki wasanii.

Diamond hakuishia katika mahojiano hayo yaliyoongoza na mtangazaji Omary Tambwe, Machi 20 kupitia mtandao wa Twitter alimjibu naibu waziri huyo akisema ametumia njia hizo kumjibu kwa kuwa naye alitumia hizo hizo.

Hata hivyo, jana mamlaka za Serikali ikiwamo Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na Waziri wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe walimshukia mwanamuziki huyo wakisema amefanya makosa kumshambulia naibu waziri kwa kuwa uamuzi anaotoa siyo wake binafsi.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Diamond Platinumz umejipanga kupambana na serikali? maana vihela ulivyonavyo vinakupa jeuri

    ReplyDelete
  2. Binafsi kama namuelewa sana Diamond maana kasema mambo mengi sana tena yenye tija ila sema hili swala limekuwa Personal sana kwa waziri husika na zaidi Mondi kasema kila alichotaka kusema ili mambo yakae sawa moyoni mwaka. Tatizo la Watanzania hawapendi kusikia na kuambiwa ukweli maana the way waziri husika alivyo adress suala lenyewe na Diamond katumia njia hiyo hiyo sasa sijajua kuzalilishwa wanakosema ni kupi ? Kiukweli mi kama sielewi hawa viongozi wetu wanataka nini, au ndo zile kunya anye kuku akinya bata basi kaharisha. Mondi mi namuunga mkono asilimia mia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad