Diamond Platnumz Aweka Wazi Mipango yake ya Ndoa

Msanii wa muziki mwenye mafanikio makubwa hapa nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ ameweka wazi mipango yake ya ndoa huku akiomba baraka kutoka kwa mama yake mzazi.

Diamond ameandika katika ukurasa wake wa instagram akimtakia mama yake heri ya siku ya wanawake ambpo amemshukuru kwa malezi aliyompa tangu akiwa mtoto mdogo.

“Happy Women’s day Mama na wanawake wote Ulimwenguni… Nashkuru sana kwa kunizaa na kunilea…Wewe ni Mboni na Nguzo ya Maisha yangu mama…Licha ya shida na Mateso uliyoyapata kwenye kunizaa na kunilea, lakini hata sasa ambapo ulitakiwa walau Upumzike nimekuwa nikikukosea kwa kukuingiza hata kwenye Matatizo Yasiyokuhusu…Wanakutukana, wanakukebehi na kukutupia kila neno lililo baya, yote kwa sababu yangu mimi, lakini sikuzote umekuwa mwenye kunisamehe, kunipenda na Kunithamini…..Nakupenda sana Mama, Na nisameh kwa yote nilokukosea… Inshaalah, Mwenyez Mungu anibariki Mwaka huu Mwanao nifanikishe Ndoa yangu na kukupa Furaha ya Milele ambayo siku zote umekuwa Ukiitaka….. @mama_dangote

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad