Esma Afunguka Busu Tata Alilopigwa na Wema Sepetu " Busu Alonipiga Wifi Yangu ni Kwasababu Tunapendana"

Esma Afunguka Busu Tata Alilopigwa na Wema Sepetu " Busu Alonipiga Wifi Yangu ni Kwasababu Tunapendana"
DADA wa mwanamuziki maarufu wa Afro- Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Abdul amefungukia busu alilopigwa na staa wa filamu ambaye amewahi kuwa wifi yake kwa kaka yake huyo, Wema Sepetu kuwa lilikuwa ni la kawaida tu kwani wanapendana sana.

Akizungumza na Ijumaa, Esma alisema hakuona kama kuna tatizo lolote kupigwa busu na Wema kwa sababu ni kitu ambacho wamekizoea siku nyingi tangu walipokuwa mawifi kwa hiyo kwao siyo kitu kigeni ni mambo ya kawaida tu.

“Busu alilonipiga wifi yangu ni la kawaida kabisa hakuna kitu kipya hapo ni upendo tu kwa sababu mimi na yeye tunapendana sana ndiyo maana umetuona hata kwenye busu hilo hatuna shaka na mtu,” alisema Esma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad