Faiza: Siwezi Kwenda Kumuona Sugu Wala Kumpeleka Mtoto Akamuone Baba Yake Gerezani

Faiza: Siwezi Kwenda Kumuona Sugu Wala  Kumpeleka Mtoto Akamuone Baba Yake Gerezani
MWIGIZAJI wa Bongo Movies ambaye ni mzazi mwenza na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi almaarufu Sugu, Faiza Ally amefunguka kuhusu kumpelekea mtoto gerezani kumuona baba yake huyo alikofungwa kwa miezi mitano.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kumpeleka mwanaye akamuone baba yake gerezani Mbeya na kumjulia hali, Faiza alisema kuwa, hawezi kufanya hivyo kwa kuwa Sugu siyo ndugu yak


“Siwezi kwenda kumuona Sugu wala kumpelekea mtoto akamuone gerezani kwa sababu kwanza siyo ndugu yangu, siyo rafiki yangu na siyo mpenzi wangu. Mapenzi yalishaisha zamani, amebakia kuwa baba wa mtoto, basi, hayo mengine siwezi kuyafanya kwa kweli,” alisema Faiza.

Sugu yupo katika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya akitumikia kifungo cha miezi mitano aliyohukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad