Fatma Karume Ajitosa Kumrithi Tundu Lissu Urais TLS


Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume amejitosa kumrithi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa kugombea urais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), utakaofanyika Aprili 14, mwaka huu.

Lissu, ambaye aliteuliwa kugombea nafasi hiyo lakini ameshindwa kukidhi matakwa ya kamati kutokana na fomu ya uteuzi iliyowasilishwa kwa sekretarieti hiyo.

Kwa mujibu wa sheria mpya, Lissu hataweza kugombea tena nafasi hiyo kwani kifungu cha nane cha sheria hiyo, kinamzuia mtu ambaye ni kiongozi wa chama chochote  cha siasa, kuongoza chama hicho.

Katika kinyang’anyiro hicho, Fatma atachuana na Godwin Mwapongo, Godfrey Wasonga na Godwin Ngwilimi huku nafasi ya umakamu wa rais ikiwa na mgombea pekee, Rugemeleza Nshalla na Mweka Hazina akiwa Sadock Magai.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uteuzi wa chama hicho, Dk. Kibuta Ongwamuhana, uchaguzi wa rais utatanguliwa na viongozi wa kanda utakaofanyika kila mkoa kuanzia Machi 27, mwaka huu.

Wakizungumzia uchaguzi huo baadhi ya mawakili wamesema wanamtabiria Fatma ushindi wa kishindo kutokana na kuwa na kariba inayofanana na Lissu.

“Fatma atashinda kwa sababu anapenda mtu mwenye ‘tension’ na ni mtu mwenye kujiamini anaweza akaitetemesha serikali na wanasheria wanapenda hivyo,” amesema mawakili wa kujitegemea ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Wakili mwingine alisema ingawa sheria hiyo inamkataza Lissu kugombea ambapo walipanga kumchagua tena mwaka huu lakini Fatma anaweza kuziba pengo la Lissu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad