Gazeti la Tanzanite Kitanzani kwa Habari zisizo na ueledi. Waitwa ofisi ya Habari Maelezo Kujieleza

Leo kwenye mitandao ya kijamii imesambaa nakala ya gazeti la Tanzanite inayotarajia kutoka siku ya Jumatatu(Kesho) yenye maudhui yanayokinzana na maadili ya kitaaluma yanayomzungumzia mwanadada Mange Kimambi, kutokana na hilo, Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali imepata malalamiko na kuamua kuita wahusika kuja kutolea maelezo.


Ameandika Msemaji Mkuu wa Serikali, nanukuu
''Nimepokea malalamiko mengi kuhusu maadili ya kitaaluma katika toleo linaloonekana mtandaoni la gazeti la Tanzanite.Gazeti hili limesajiliwa kutoka kila jumatatu,hivyo tumewaita wahusika kesho baada ya kuona nakala halisi ili kupata maelezo yao.''
Source:Jamii Forums
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad