Simba iko mjini hapa kuivaa Al Masry katika mechi ya Kombe la Shirikisho lakini hali ya baridi na hasa jioni inaweza kuwa tatizo kwa Simba.
Hali ya nyuzi joto 17 wakati wakiwa wametoka jijini Dar es Salaam ambako kuna nyuzi joto hadi 33.
Hata hivyo, inaonekana kufika mapema mjini hapa inaweza ikawa faida zaidi kwao kwa kuwa watafanya mazoezi zaidi ya mara mbili.
Simba walionekana wakiwa na uchovu wa safari tangu mara tu baada ya kuwasili mjini hapa na Kocha Mfaransa, Pierre Lechantre alitoa nafasi ya wachezaji wake kupumzika kwanza kabla ya kuanza maandalizi tena.
Hali ya hewa ya baridi kali si nzuri kwa wachezaji wa Simba ingawa wenyeji wanaona baridi ni kama vile imeisha na si kali ambako hufikia wakati mwingine hadi nyuzi joto 5.