HAWA Watu Ndani ya Serikali Hawamuogopi Mungu - Prof Tibaijuka

Mbunge wa Muleba Kusini(CCM), Anna Tibaijuka amefunguka na kusema kuwa wapo watu ndani ya Serikali ya awamu ya tano hawamuogopi Mungu ndiyo maana wanakuwa wanawaonea wananchi na kuichafua serikali pamoja na Rais Magufuli.


Tibaijuka amesema hayo wakati akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara baadaa ya kuona watu wakilipishwa kodi na kupewa risiti za mwaka 2015 fedha ambazo zinaonekana hazifiki serikalini.

"Serikali ya Rais Magufuli haiwezi kukubali haya mambo wanataka tu kuchafua jina la Rais amini usiamini serikali zinahujuma ndani yake sasa watu wanatokaje Mwanza na kumlazimisha huyu mvuvi mkubwa ambaye ana mitumbwi 28, anakuja mtu mla rushwa serikali ya Magufuli haiwezi kumtoa mtu kule aje kula rushwa huku, Rais Magufuli huyu anayelia usiku na mchana mambo yakae vizuri ila leo nitamtumia risiti zile za watu wake wamekusanya kodi hapa kwa risiti za mwaka 2015" alisema Tibaijuka 

Aidha Tibaijuka amesema kuwa yeye anaamini kuwa Rais Magufuli hawezi kutuma watu kwenda kuchoma nyavu za wavuvi

"Yaani wamemkuta mvuvi yupo stoo anaendelea na mafundi wake kurekebisha hawa watu ambao hata hawamuogopi Mwenyezi Mungu wanaingia mle stoo na kuchoma zile nyavu, sasa watu wanasema siku za mwizi arobaini" alisema Tibaijuka 
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ah mama wee hata haya huna kumtaja Mwenyezi Mungu je wewe na zile"Eti milioni kumi hela ya mboga tu"wakati zimeingia katika akaunti yako kulikuwa hakuna Mungu au?Acha bla bla zako

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad