Hii ndiyo Chocolate ya Gharama zaidi Duniani

Basi jana March 16, 2018 chocolate inayodaiwa kuwa ya gharama ya juu zaidi duniani ilipelekwa kwenye maonyesho ya biashara kwenye Mji wa Obidos nchini Ureno.

Chocolate hiyo ambayo ni ya gharama ya Euro 7,728 ambayo ni sawa na Fedha za Kitanzania Shilingi Milioni 20.7, imefunikwa na dhahabu inayoweza kuliwa, na imetengenezwa na vitu vingine ikiwa ni pamoja na truffle nyeupe, nyuzinyuzi za saffron, na vanilla kutoka Visiwa vya Madagascar.

Mtengenezaji wa chocolate hiyo Daniel Gomes ambaye ni raia wa Ureno ameeleza kuwa chocolate hiyo ambayo ina umbo la fedha imepewa cheti cha kutambuliwa kama Chocolate ya gharama ya juu zaidi duniani na Kitabu cha Kumbukumbu cha Guiness mwaka 2017.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad