Hiki Hapa Kilichojili Kwenye Kesi ya Rugemarila

Hiki Hapa Kilichojili Kwenye Kesi ya Rugemarila
Mahakama ya Rufani imesikiliza maombi ya mfanyabiashara James Rugemarila kuhusu kurekebisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa ya kupinga kunyimwa dhamana na Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ‘Mahakama ya Mafisadi’.

Maombi hayo yamesikilizwa mbele ya Jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Bernad Luanda, ambapo wengine ni Batuel Mmilla na Gerald Ndika.

Katika maombi hayo ambapo Rugemarila amejiwakilisha mwenyewe anaomba mahakama imruhusu kufanya mabadiliko ya kusudio la kukata rufaa kuhusu dhamana yake.

Pia imruhusu amuingize mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi kama mtu muhimu katika maombi hayo.

Pia mahakama hiyo impatie dhamana wakati maombi hayo yakiendelea kusikilizwa.

Katika maombi hayo upande wa Jamhuri umewakilishwa na Mawakili wanne, akiwemo Zainabu Mambo na Tumain Kweka ambao wamepinga kupokelewa kwa maombi ya Rugemarila.

Akitoa hoja za kupinga kupokelewa kwa maombi hayo, Wakili Kweka ameomba maombu hayo yatupiliwe mbali kwa sababu yamefunguliwa kupitia kifungu kisicho sahihi ambacho kinaichanganya mahakama kujua kama yamefunguliwa kama kesi ya jinai ama madai.

Pia mfanyaniashara Seth ameingizwa kimakosa katika maombi hayo, hivyo hausiki kwa sababu maombi yake dhamana Mahakama Kuu yalitupiliwa mbali, hivyo alipaswa kufungua maombi mengine katika Mahakama ya Rufaa na sio kujumuishwa katika maombi ya Rugemarila.

Kutokana na hoja hizo, Rugemarila naye ametoa hoja zake akidai kuwa maombi yake yapo sahihi na anaiomba mahakama iyapokee.

“Pingamizi la Jamhuri halipo sahihi kwa sababu hawajafafanua ipasavyo kwa kile wanachokipinga, pia walipaswa kutoa pingamizi hilo kwa njia ya maandishi,”.

Kuhusu suala la kumuingiza Sethi, Rugemarila ameiomba mahakama iyapokee kwanza maombi yake kisha wakati wa kusikilizwa ndipo ataeleza sababu za kumuunganisha.

Baada ya kueleza hayo, Jaji Luanda amesema wanaahirisha maombi hayo na watapanga tarehe kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Kwa pamoja washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad