Hili Hapa Swali la Lema Leo "Ni kweli Tunahitaji Kamati Teule Kuhusu Utekaji ?

Hili Hapa Swali la Lema Leo "Ni kweli Tunahitaji Kamati Teule Kuhusu Utekaji ?
Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema amesema wanapita katika maumivu makali katika siasa wanazozifanya hivyo hawaitaji kuona sinema tena zikiendelea kutoka kwa miongoni mwa wabunge wenzao.

Hiyo inakuja baada ya Mbunge Hussein Bashe kupelekea barua hiyo kwa Katibu wa Bunge kutaka iundwe kamati Teule ya kuchunguza baadhi ya mambo yanayoendelea nchini.



Lema ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram amehoji kuwa Hivi ni kweli tunahitaji Kamati teule kuhusu utekaji na kufifia kwa demokrasia Nchini ?.

Nina fikiri ninapaswa kusema kidogo juu ya hoja binafsi ya Mh Husein Bashe katika mkutano wa Bunge unaokuja.Hivi ni kweli tunahitaji Kamati teule kuhusu utekaji na kufifia kwa demokrasia Nchini ?

Ni maamuzi ya ccm ktk mikutano yao ya ndani ya Bunge na nje ya Bunge kuhusu hali ya demokrasia na siasa Nchini, ujenzi wa vyama vya siasa na mikutano imepigwa marufuku .

Mikutano ya Bunge live pia imepigwa marufuku , Wabunge na Madiwani wa Upinzani waneendelea kupitia mateso makubwa,vitisho vya mauaji , kuwekwa mahabusu na kufungwa.

Wakati mambo haya yanaendelea kutokea Bunge limekataa hata kulipa matibabu ya Mh Lissu.
Hakuna Mbunge mmoja wa ccm akiwemo Husein Bashe alishawahi kwenda kumjulia hali Mh Lissu Hospital, unajiuliza ni kwa nini ?

Mambo haya yako wazi hayahitaji PHD kujua msimamo wa Wabunge wa ccm kuhusu haki,ukweli na nuru ya mabadiliko .

Wabunge wa ccm wakibadili mtazamo kuhusu Nchi Bunge litakuwa imara na Bunge imara ndio msingi wa Serikali bora na Bunge imara linatokana na Wabunge majasiri, wako wapi ndani ya ccm ?
Msingi wa kwanza wa ukomavu wenu ni kurudisha hadhi ya Bunge kwa umoja na idadi yenu , platform nyingine nje ya kujitathimini kwa masilahi ya Nchi ni unafiki.
Bashe unafikiri Kamati teule inaweza kuwa na maana kwenye Bunge hili ? hotuba za Wapinzani Bungeni zime endelea kuwa sensored ndani ya Bunge na haya ni maoni mbadala ya ushauri kwa Serikali lakini siku zote mmekaa kimya.

Chama chako ni tatizo na Viongozi wake,na wewe unafahamu mambo haya, hivi kweli tunahitaji tena kugundua kanuni ya kutengeneza gari wakati kuna magari yana tembea barabarani ?
Tunahitaji umoja wenu kwa masilahi ya haki ndani ya Bunge kwenye mambo yote yanayo rudisha heshima ya Wabunge , wingi wenu umekuwa hasara kwa Nchi badala ya faraja.

Tunapoona maigizo yanayotaka kupotosha haki yanazingatiwa hapa ndipo tunapatwa hasira na kuondoa nidhamu katika mahusiano yasiyo na tija na Nchi , hata hivyo andiko hili sio ugomvi lakini pia limejengwa hasira na hali zetu kisiasa tunayopitia, sisi Wabunge wa upinzani karibu wote tuna kesi sehemu mbali mbali Nchini, mmoja wetu sasa ni mfungwa (Sugu) .

Tunapitia maumivu makali sana kwa sasa hatuitaji tena sinema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad