Hizi Hapa Aina Mbali Mbali za Hasira za Mwanamke...Tahadhari


1. Kuna mwanamke ambaye akikasirika, huishia kulia tuu!

2. Lakini mwingine akichukia, anaongea saanaa muda wote hadi ikukere!

3. Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. Shavu limejaa kama Kobra!

4. Mwingine akishikwa na hasira, period ya ghafla ghafla inafuata!

5. Wako wanawake ambao, ole achukie! Atakachokishika usipokimbie anakutandika nacho, majuto baadaye! Baba mmoja alipigwa 'Pedi' ilotumika, kufuatia kung'ang'ania tendo, huku mwenzi wake yuko katika hali hiyo!

6. Mwanamke mwingine akikasirika, hasira zake zinaishia kwenye kuvunja-vunja vyombo. Au saa nyingine kugombeza-gombeza wafanyakazi na watoto! Dizaini hii, huwa ni wale waliokosa kukidhiwa haja za kihisia na waume zao!

7. Mwanamke mwingine ole akasirike. Mtajuana kitandani panapo majaaliwa! Nakwambia utaungama yote!

8. Kuna ambao wakitibuliwa, hukimbilia kufunga mabegi na kuondoka!

9. Wapo ambao wakikasirika, wanagoma kupika!

10. Wengine wakichukia, wanaamua kwenda kulala kimyaaa!!

11. Wanawake wengine wakikasirika, tumbo linakata, na pengine mpaka kuharisha!

13. Wako ambao wakishikwa na hasira, huingia maombi na kuugua kusikoweza kutamkwa. Uchungu ukiisha, wananawa uso na kwenda sokoni.

14. Yuko ambaye akishikwa na hasira, hucheka saaanaaa.... Hutajua kama amekasirika! Dizaini hii ni hatari sana, maana anaweza kukudhuru kiurahisi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad