Hizi ndio timu ziliotinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika

NCHI za Algeria, Morocco na Tunisia zimeongoza kwa kuingiza timu kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu baada ya mechi za hatua ya 32 Bora kukamilika mwishoni mwa wiki.

Kila moja imeingiza timu mbili, Algeria ikizipitisha ES Setif iliyoitoa Aduana Stars ya Ghana na MC Alger iliyoitoa Mountain of Fire and Miracles (MFM FC) ya Nigeria.

Morocco imezipitisha Difaa Hassan El Jadida iliyoitoa As Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mabingwa watetezi, Wydad Casablanca walioitoa Williamsville AC ya Ivory Coast.

Tunisia imeingiza vigogo wake wawili, Esperance walioitoa Gor Mahia ya Kenya na Etoile du Sahel walioitoa Plateau United ya Nigeria.

Timu nyingine zilizofuzu hatua hiyo ya 16 Bora ni Angola 1º de Agosto ya Angola, Township Rollers ya Botswana, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Al-Ahly ya Misri na Horoya ya Guinea.

Nyingine ni Mamelodi Sundowns, Mbabane Swallows ya Swaziland, AS Togo-Port ya Togo, KCCA ya Uganda na ZESCO United ya Zambia.

Kutakuwa na makundi manne kila moja litakuwa na timu nne na washindi wawili wa kila kundi watakwenda Robo Fainali ya mtoano.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad