Huku Panapoelekea Ndoto ya Baba Daimond kwa Wema Zitatimia

Huku Panapoelekea Ndoto ya Baba Daimond kwa Wema Zitatimia
AWALI ya yote nikiri tu kwamba, mimi ni kati ya watu ambao walitokea kuipenda sana ‘kapo’ ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Wema Sepetu. Nilitokea kuwapenda tu. Nilisikia raha sana nilipokuwa nikisikia wakiitana majina mazuri kama vile baby…honey…sweet heart na nikatamani sana kusikia siku moja wamekuwa mke na mume.



Bahati mbaya sana ni kwamba, si kila anachotaka binadamu kitokee, kinatokea na hii inatokana na ukweli kwamba, kila jambo linapangwa na Mungu. Kama Mungu akisema hili ‘no’, hata ufanyeje haliwezi kutokea. Ila akisema liwe, basi linakuwa.



Lakini niwakumbushe tu kwamba, siyo mimi peke yangu niliyekuwa nikitaka siku moja Wema na Diamond waoane. Wapo mashabiki wengi tu ambao nao walikuwa wakitamani iwe hivyo.


Diamond na Zari.

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mitandao, utakubaliana na mimi kwamba, kila picha ya Diamond na Wema ilipokuwa ikitupiwa, wengi walikuwa wakikomenti kuonesha kuwa, wanawapenda na wanatamani wawe mwili mmoja.



Achana na mimi na hao mashabiki wengine wa mastaa hao, hata baba mzazi wa Diamond, Mzee Abdul Juma naye aliwahi kukiri kuwa anampenda sana Wema na moyo wake ungefarijika sana kama siku moja angemuita Wema mkwe wake. Kwa bahati mbaya sana uhusiano wa wawili hao ukawa mara unang’ara, mara unazimika.



Mtakumbuka Wema na Diamond wameachana na kurudiana zaidi ya mara moja. Hata hivyo, mara ya mwisho walivyoachana kasha Diamond akajiweka kwa Zarina Hassan ‘Zari’ kisha wakazaa watoto wawili, kila mmoja alijisemea kuwa, Diamond na Wema imebaki stori na hawawezi kurudiana tena.


Baba Diamond akiwa amembeba mjukuu wake.

Ghafl a mambo yamebadilika, tumeona Zari ameamua kubwaga manyanga baada ya kuona Wema amerudisha majeshi kiaina. Hata hivyo, hakuna anayeweza kuthibitisha kwamba Wema na Diamond wamerudiana lakini kuna kila dalili kwamba, wawili hao wameamua ‘kama mbwai iwe mbwai tu’. Vijana wa mjini wanasema; ‘kama kusoma huwezi hata picha nayo huoni?



Sasa kwa nini nasema ‘soon’ ndoto za Baba Diamond ‘Baba D’ zitatimia? Iko hivi, Diamond amewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mademu kibao. Kwa kifupi mtungo wa huyo dogo unawafunika mastaa wote wa kiume.



Naweza kusema Diamond ndiye staa wa kiume aliyetembea na mastaa wengi wa kike hapa Bongo. Kajiachia na Irene Uwoya, Wema Sepetu, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Jokate Mwegelo, Hamisa Mobeto na wengineo.


Diamond.

Lakini sasa katika listi hiyo, hakuna hata mmoja aliyewahi kutambulishwa kwa wazazi wote wa Diamond isipokuwa Wema na Mobeto.



Ndiyo maana hata kwa picha tu tanaona kwamba zipo picha ambazo Wema amepiga na baba Diamond na mama Diamond, Mobeto naye kapiga akiwa na wazazi wote lakini sasa kuwahakikishia kuwa, Wema ndiyo chagua la baba D, yeye tu ndiye aliyefanikiwa kupiga picha ya pamoja akiwa na Baba D na Diamond.



Niambie wewe msomaji, uliwahi kumuona Diamond na demu gani wakiwa wamepiga picha na baba Diamond? Kwa kifupi hakuna! Lakini pia kama hujui basi leo ndiyo ujue kwamba, hakuna hata picha moja inayomuonesha baba Diamond akiwa na Diamond isipokuwa picha hiyo moja tu ambayo yupo Wema, Baba D na Diamond.



Hii ina maana gan



Inaonesha kwamba Diamond alimpenda sana Wema hadi akafi kia hatua ya kumpeleka kwa ‘mdingi’ wake na kwa bahati nzuri baba naye akabariki ndoa lakini haikuwa hivyo.



Sasa Wema na Diamond wamekuwa ndiyo habari ya mjini na watu wa karibu na baba D wanasema kuwa, anaomba usiku na mchana warudiane na wafunge ndoa.



Sisi yetu macho tu ila kwa maoni yangu mimi, Wema ana kila kigezo cha kuwa mke wa Diamond, kwanza wote dini moja, wamekuwa pamoja kwa muda mrefu, wanajuana vizuri hivyo ni rahisi ‘kushikiana madhaifu’ yao na wakadumu kwenye ndoa yao. Ila yote kwa yote ni wao na maisha yao!.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ingekuwa fresh sana kama hiyo ndoto yako ingetimia na kuwa kweli walakini unajitokeza katika pande zote mbili za hao wahusika kuwa wote hawajatulia na hawatoweza kutulia kwenye relationship na partner mmoja tu kwa sababu kitabia wote wawili ni wachepukaji "maarufu" nje ya relationship kwa tabia hiyo sidhani na wala kutegemea kuja kusikia wahusika hao watakuja kuoana(mke+mume)na hata kama itakuja kutokea wakaoana swali litakuwa je hiyo ndoa yao itadumu for how long?Patamu hapo!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad