Huku Sakata la Waziri na Diamond Platnumz Likishika Kasi, Diamond Aweka Rekodi YouTube Barani Afrika

Diamond Platnumz kila kukicha anaendelea kuweka rekodi kwenye muziki wake na awamu hii sio views wa kwenye mtandao wa YouTube bali ni Subscribers.

Diamond kwenye akaunti yake ya YouTube tayari amefikisha Subscribers milioni 1+ na kuwa msanii wa muziki wa 8 barani Afrika kuwa na Subscribers zaidi ya milioni 1.

Kwa sasa Diamond Platnumz ameungana na wasanii kama Amr Diab kutoka Misri mwenye Subscribers milioni 1.6, Kundi la muziki la Die Antiwoord kutoka Afrika Kusini subscribers milioni 1.8, Dzjoker Chemsou milioni 1.6, Lartiste milioni 2.2, Ilias Tiiw milioni 1.8, Sofia Carlsberg milioni 1.8 .

Wengine ni Tamar Hosny milioni 2.8, shady Srour milioni 2.8 wote kutoka Misri na Saad Lamjarred kutoka Morocco ambaye ndiye msanii wa muziki anayeongoza kwa bara la Afrika kuwa na Subscribers wengi milioni 4.4 .

Kwa upande wa wasanii wengine kutoka Afrika kama Davido, Wizkid, Yemi Alade, Tiwa Savage, Sarkodie, Alikiba na Cassper Nyovest wote bado hawajafikisha Subscribers milioni 1 ingawaje hao wanatumia mtandao wa VEVO, na akaunti inayoongoza kuwa na Subscribers wengi ni ile ya kundi la PSquare ina subscribers laki 7.

Wiki iliyopita Diamond Platnumz aliachia album yake ya ‘A BOY FROM TANDALE’ na tayari imepokelewa vizuri na mashabiki wa muziki barani Afrika ambapo imeanza kutrend kwenye mitandao ya kununulia nyimbo kwenye baadhi ya nchi kama Burkina Faso, Oman, Namibia, Kenya, na Malaysia na kwenye mitandao mikubwa ya kimuziki kama SPOTIFY

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad