Huyu Ndio Paka Anayeharibu Mimba kwa Wanawake

Huyu Ndio Paka Anayeharibu Mimba kwa Wanawake
Daktari wa wanyama nchini Tanzania, Dkt. Obed Kiariro amedai kuna uwezekano mkubwa wa Paka anayefugwa majumbani hupelekea kuharibu ujauzito kwa binadamu endapo mnyama huyo hatopewa matunzo mazuri yanayostahili kwa wakati.


Dkt. Kiariro ameeleza hayo kupitia kipindi cha Supamix kinachorushwa na East Afrika Radio baada ya kuwepo matatizo mengi wanayoyapata jamii ya kike (wanawake) hasa hasa pale wanapokuwa wamebahatika kushika ujauzito na kwa bahati mbaya hutokea kuharibika bila ya kujua sababu za msingi kilichopelekea kupoteza ujauzito wake.

"Kuna ugonjwa tunaita 'toxoplasmosis' kitaalamu ugonjwa huu unatoka kwa Paka ambao unapelekea kutoka kwa mimba 'abortion', kama Paka hawatibiwi vizuri wala kuwepo na matunzo ya aina yeyote basi wanakuwa na ugonjwa huo na matokeo yake wanaambukia wanadamu. Unaweza ukawa na paka nyumbani unamtunza vizuri lakini huwezi kumzuia kwa namna yeyote ile kutokutana na paka wengine wanaozurura mtaani maana wakikutana tu wanaambukizana ugonjwa huo", amesema Dkt. Kiariro.

Mtazame hapa chini Dkt. Kiariro akielezea vizuri namna ya paka anayesababisha kuharibika kwa ujauzito (mimba).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad