Ifahamu sheria ya maandamano Kikatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Maandamano ya aina yoyote ni haki ya mwananchi na yanaruhusiwa kisheria lakini maandamano hayo lazima yafuate sheria na taratibu zilizobainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sheria ya maandamano inamtaka mwananchi au kundi la wananchi wanaohitaji kufanya maandamano kutoa taarifa kwa maandishi kwa Mkuu wa Polisi wa eneo husika kabla ya masaa 48 ya kuanza kwa maandamano hayo ikieleza dhumuni la maandamano hayo.

Pia wahusika wanatakiwa wawe tayari kwa jibu lolote kutoka kwa mkuu huyo kwa kuwa chochote watakachojibiwa lazima kiwe na sababu.

Endapo wahusika watakataliwa kufanya maandamano na hawatoridhishwa na sababu zilizotolewa na Mkuu wa Polisi kuna hatua mbili muhimu zinazotakiwa kufuatwa na sio wahusika kujiamulia kuandamana kilazima kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa.

Hatua hizo muhimu zinazotakiwa kufuatwa ni kuandika barua kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kumueleza kutoridhishwa na sababu zilizotolewa na Mkuu wa Polisi ili Waziri naye kwa upande wake aamue kuruhusu au kukataza.

Endapo wahusika hawatoridhika na majibu ya Waziri, waandamanaji watatakiwa kwenda Mahakamani ambapo ndipo uamuzi wa mwisho utatolewa.

Hakuna sheria inayotambua maandamano ya nchi nzima kufanyika kwa siku moja kwa sababu kila eneo lina Mkuu wa Polisi mwenye haki ya kukubali au kukataa ombi la kufanya maandamano kulingana na hali halisi ya eneo lake.

Kila jambo lina faida na hasara zake lakini kuna mambo ambayo faida huwa chache kuliko hasara, maandamano yana athari kubwa kiuchumi na kijamii kwa sababu maandamano yoyote ni lazima Jeshi la Polisi liwajibike katika kuongoza na kulinda maandamano hayo, hivyo kupelekea wanajeshi wengi kusitisha kazi zingine kwa ajili ya kuzuia vurugu zisitokee.

Athari zingine ni kusitishwa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za usafiri , kufungwa kwa maduka na masoko pamoja na athari zitokanazo na vurugu zinazoweza kutokea kwa sababu ya maandamano hayo.

Hivyo itambulike kisheria hatua hizo zinatakiwa kufuatwa kabla ya kufanya maandamano, aidha maandamano kisheria ni jambo halali endapo tu litakuwa limehalalishwa kisheria.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sasa kwa maelezo ya hapo juu utaona jinsi gani viongozi wa upinzani hasa Chadema wanavyopotosha Umma na kuwapelekea wananchi kuvunja sheria. Kwa utaratibu uliotajwa hapo juu ni wa kuvutia mno na wenye kuepusha mvutano kama watu watafuata sheria. Wakati mwengine kwa kweli utaona hatuhitaji katiba mpya,katiba iliopo inatosha ila ifanyiwe maboresho, ni kupoteza muda na pesa za watanzania kugharamia mchakato mzima wa katiba. Watanzania tunachohitaji ni viongozi wapya na sio katiba mpya hasa kwa upande wa upinzani. Kwa viongozi hawa upinzani tulinao sasa hata hiyo katiba mpya ikipatikana kazi bure. Viongozi karibu wote wa upinzani ukiangalia mitazamo yao ya kisiasa ni ya upotoshaji zaidi wa hali halisi ya mambo kunako lenga kuwahamasisha wananchi katika kuvunja sheria za nchi. Katika maandamano amabayo u. yaliosababisha kifo cha mwanafunzi hivi karibuni utaona viongozi wa Chadema waliamua hafla kufanya maandamano kitu amabacho ni dhahiri kilikuwa ni uvunjifu wa sheria. Kutokana na maelezo ya hapo juu nimejufunza kitu kimoja cha maana sana leo. Mara nyingi nimekuwa nikiwalaani polisi kuzuia maandamano lakini leo nimejua kumbe wapo right. Huwa wanfuata sheria za nchi siku zote sikuufahamu utaratibu unaotakiwa kufuatwa ili kufanya maandamano. Kwa mfano maandamano ya Chadema yaliouwa mwanafunzi hivi karibuni kiuhalisia huwezi kuwalaumu polisi kwa sababu Chadema na viongozi wake walishindwa kufuata sheria kuitisha maandamano yale na moja kwa moja kuliwapelekea polisi kuchange their mind set kutoka kusimamia maandamano ya amani na kushughulikia suala la uvunjifu wa sheria za nchi. Katika kusimamia uvunjifu wa sheria za nchi polisi na vyombo vengine vya dola Duniani kote huwa wapo tayari lolote lile kuhakikisha hali inarudi na kuwa ya kawaida. Chadema wanapaswa kuadhibuwa kwa kufanya maandamano yale haramu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad