Katika maisha yako yote ambayo utaishi hapa dunia basi tambua ya kwamba bila kuwa mbunifu basi utaendelea kuungua na jua maisha yako yote, nasema hivyo nikiwa na maana ya kwamba asilimia 99.99 ili uweze kupiga hatua za kimafanikio kila wakati katika maisdha yako ni lazima uwe mbunifu.
Ubunifu ndio nguzo nambari moja ambayo itakufanya wewe kuweza kufanikiwa, ikiwa hautajenga misingi ya ubunifu katika jambo lolote ambalo unalifanya basi ni kwamba utaendelea kuishi maisha ya kawaida na matokeo ambayo utayapata nayo tayakuwa ni ya kawaida tu.
Kwa sababu katika karne hii kwa asilimia kubwa kitu ambacho unakifanya wewe kwa asilimia kubwa ni lazima kitafanana na mtu mwingine, kama ndivyo hivyo basi ikiwa mfanano wa vitu unazidi kuongeze swali la msingi ambalo unatakiwa kujiuliza ni, hivi natajitautishaje na wenzangu?
Majibu ya swali hilo ni kwamba ili kujitofautisha kivingine unachotakiwa kufanya ni kuhahahakikisha ubunifu unahusika kwa asilimia kubwa. Mtu mwingine anaweza kuja kifua mbele akaniuliza sasa afisa mipango huo ubunifu ni nini? Pasipo kuona haya endapo niutaulizwa swali kama hilo jibu ambalo nitampa nitamwambia, ubunifu ni kuongeza thamani kwa kitu ambacho unakifanya, aidha kama utashindwa kuongeza thamani basi utakiwa kuunda kitu kipya.
Katika swala kuunda kitu kipya hapa ndipo pamekuwapo na tatizo fulani kwa sababu watu wengi wanapenda sana ganda la ndizi kuleteleza, kwa maneno mengine tunaweza kusema akili zao zimeganda hasa katika suala la kufikiria wao wamekuwa wanapenda sana kufanya copy & paste. Kufanya hivyo ni kujipoteza mwenyewe hivyo unachotakiwa kufanya ni kwamba lazima uwe na misingi ya kubuni kitu cha kwako.
Pasipo kupoteza kusudio la mada yangu ya siku ya leo, niliona ni vyema niianze na utangulizi huo ili uelewe maana ya ubunifu. Mara baada ya kufahamua maaana ya ubunifu basi naomba japo kwa dakika chache tuangalie misingi ya ubunifu kama ifuatavyo.
1. Ukitaka kuwa mbunifu katika eneo lolote lile , kwanza ni lazima uhakikishe unafanya kitu ambacho unakipenda. Ukifanya kitu ambacho unakipenda kwa asilimia zote, upo uhakika wa asilimia zote kwamba ni lazima utakuwa mbunifu ili kuwashinda washindani wako wanakuzunguka.
2. Ili uweze kuwa mbunifu katika jambo ambalo unalifanya jambo jingine ambalo unatakiwa kulizingatia ni kwamba ipo haja kubwa sana ya kuwekeza muda mwingi katika kuliwaza na kulitenda jambo hilo. Hivyo kwa kuwa umeamua kuyasaka mafanikio kwa udi na uvumba huku ukiamini ya kwamba ubunifu ndiyo ambao utakusaidia kuwa hivyo basi hakikisha ya kwamba unajipanga kikamilifu kuweza kujitoka kwa kuwekeza muda wako mwingi ili kuweza kulitimiza jambo hilo.
3. Jambo jingine ambalo litakufanya wewe uweze kuwa mbunifu ni kwamba ni lazima uhakiishe ya kwamba kila wakati huchoki kujifunza vitu vipya ambavyo vinaendana na jambo hilo. Samabamba na hilo kwa kuwa binadamu kwa asilimia kubwa kuna uwezekano mkubwa sana wa kile alichojifunza kuweza kusahau, hivyo kwa kile ambacho unajifunza ni lazima uhakikishe ya kwamba unakiandika na uwe unakipitia mara kwa mara ili usikishau.
4. Jambo la mwisho kati ya mengi yahusuyo somo hili ni kwamba kila wakati ni lazima uwe ni mtu wa kujiuliza maswali ya mara kwa mara. Moja kati ya swali muhimu ambalo unapaswa kujiuliza wewe katika misingi hii ya ubunifu ni, Je hivi nikifanya jambo hili nitapata faida gani?