Ireland Kuhalalisha ‘Utoaji Mimba’ kwa Kura

Ireland Kuhalalisha ‘Utoaji Mimba’ kwa Kura
Nchi ya Ireland ambayo ni ya misingi ya kidini hususani kwa dhehebu za Kikatoliki, suala la utoaji mimba kwa miaka mingi limekuwa haramu hata kama ni kwa kesi za kidaktari.

Kutokana na marufuku hiyo ya kisheria wanawake wamelazimika kwa kipindi chote kwenda kutibiwa nchi za nje endapo madaktari watasema inabidi watolewe mimba hizo kutokana na kuhatarisha maisha yao .

Hali hii imeanza kubadilika ambapo wanaharakati kwa miaka wameshinikiza kufutwa kwa sheria hii na kuhalaisha utoaji wa mimba kwa wanawake, na jana March 28, 2018 Waziri wa Afya nchini humo Simon Harris amezungumza.

Waziri huyo ameeleza kuwa May 25, 2018 itapigwa kura ambayo ndiyo itatoa hatima ya kuhalalishwa kwa sheria mpya ya utoaji wa mimba nchini humo baada ya miaka 35 au la.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad