Jamii Inakosa Muelekeo na Kukosa Haki Wanafunguliwa Kesi Wakubaliane na Uovu wa Kimfumo - Padre Shio

Jamii Inakosa Muelekeo na Kukosa Haki Wanafunguliwa Kesi Wakubaliane na Uovu wa Kimfumo - Padre Shio
Padre Riziki Shio wa Kanisa la Minara Miwili Zanzibar amefunguka na kusema kuwa jamii inakosa mwelekeo na kukosa haki huku wengine lukuki wanafunguliwa kesi ili wakubaliane na uovu wa kimfumo.


Padre Riziki Shio wa Kanisa la Minara Miwili Zanzibar aliyasema hayo jana Machi 31, 2018 katika ibada ya Ijumaa Kuu na kusema kuwa wapo watu wachache au wenye uwezo hukandamiza haki za wanyonge jambo ambalo ameliita uovu wa kimfumo.

"Mateso ya kimfumo ni pale wachache au wenye uwezo wanapokandamiza haki za wanyonge na hasa wale wanaoonekana kuwa mwiba katika maslahi yao, ndugu zangu mataifa mengine popote pasipokuwa na amani tunashuhudia watu wanavyouwawa, wanavyovyamiwa. Mwaka jana tulishuhudia askari wetu kule Congo walivyouwawa wakilinda amani, wao walienda kulinda amani lakini waliuwawa na watu wasiopenda amani"

Padre Riziki aliendelea kusema kuwa

"Wapo wengine huwekwa hata maabusu kwa muda mrefu bila kupelekwa mahakamani kwa vile wamesimama katika ukweli kwa hiyo jamii kama wakati wa Yesu inakosa mwelekeo, ina kosa haki, wengine wanafunguliwa kesi lukuki wakubaliane na uovu wa kimfumo"
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sasa makanisa yamegeuka kuwa majukwaa ya kisiasa. Ukristo uliingizwa nchini na wakoloni na Zanzibar hasa ndio miongoni mwa vituo vya mwanzo kabisa vilivyohusika katika kusamabaza ukristo Tanzania.Lakini kihistoria ukristo ulitumika na wakoloni kama Gia ya kumuingilia Mwafrika kisaikolojia ili kumtawala na kweli gia hiyo ya udini ndio iliyowamaliza waafrica na kujikuta wanatwaliwa na wazungu kwenye ardhi yao. Wazungu au wakoloni walikuja katika nchi zetu kama wamissionaries kuhubiri Biblia lakini kiukweli katika wamissionary hao, wengi wao walikuwa makechero waliokuwa na lengo jingine kabisa. Zama zimepita lakini inaonekana kabisa kazi ya kanisa kwa baadhi ya mataifa ya kigeni na wamissionary wao wa kigeni na ndani bado hazija badilika. Hawa wamishinari ni watumishi wa kizungu wenye extra mind of thinking,na ndio maana watumishi hawa wanaofanya kazi zao vivulini wanawaita intelligents kwa maana yakwamba kuwa ni watu wenye maarifa ya ziada kumzidi mtu wa kawaida. Mara nyingi watu wa namna hii kwa kumtizama kwa macho matupu utamuaona ni mjinga katika wajinga. Hasa ujinga wao umejiigemeza katika ukarimu. Utashangaa unaweza kuona mzungu kakuta wenyeji wanakula kinyesi nae anaungana na wenyeji kukichapa kinyesi hapana shaka wenyeji lazima watamkubali tu kuwa ni mwezao. Sasa kwa kauli za hivi karibuni za viongozi wa dini yaani Maaskofu inaonekana kabisa kanisa linatumika kisiasa Tanzania, na kwa bahati mbaya ni jambo la hatari sana kwa nchi kama Tanzania kwani ukristo sio Dini inayotwala Tanzania, Kuna uislamu, Mahindu na kadhika. Lakini inaonesha kabisa kuna nguvu fulani inataka kulitumia Kanisa kuingilia shughuli za kiserikali na ni jambo la hatari sana . Zama zimepita na inawezekana kabisa Kanisa kwa kutumia wahisani wake bado wana ajenda zile zile za umissionary katika staili mpya lakini watanzania sio wale wale wa zama zilizopita kwani taasisi za dini na mahubiri yake zinajulikana na Taasisi za kisiasa na mahubiri yake pia zinajulikana . Kwa bahati mbaya kanisa limekuwa ulingo wa siasa kwa sasa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad