Kamanda
wa polisi Mkoa wa Dodoma Giles Muroto akizungumza na waandishi wa
habari mjini Dodoma , amesema katika msako uliofanywa tangu Februari 28
mwaka huu, wamefanikisha kukamatwa kwa wahamiaji wawili na watoto hao
ambao wamekuwa wakitumia dawa za kulevya aina ya gundi.
Kamanda huyo amesema wazazi wa watoto hao wanapaswa kufika kituoni kuwachukua watoto hao ili kuepusha kushtakiwa kwa mujibu wa sheria kwa kushindwa kuwalea watoto wao.
Aidha amesema pia katika msako huo jeshi hilo limewakamata wahamiaji haramu wawili februari 28, mwaka huu ambao ni raia wa Rwanda katika 'check point' ya polisi mtera wilayani Mpwapwa barabara ya kuelekea Iringa.