Jeshi la Polisi Lakanusha Kuhusika na Kifo cha Kijana Allen Mapunda Huko Mbeya


MBEYA: Jeshi la Polisi limeutaarifu umma wa Watanzania kuwa halihusiki kwa namna yoyote na kifo cha kijana Allen Mapunda(20) anayedaiwa kufariki saa chache baada ya kutoka Kituo cha Polisi.
-
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga amewaambia Wanahabari kuwa, Jeshi hilo limeanza kufanya uchunguzi wa kina kuhusu kifo cha kijana huyo
-
Kamanda Mpinga amesema kijana huyo aliachiwa na Jeshi la Polisi muda wa saa nne asubuhi baada ya kudhaminiwa na ndugu zake na ilipofika saa 12 jioni zilipatikana taarifa kuwa mtuhumiwa huyo amefariki dunia
-
Jeshi la Polisi linatuhumiwa na Wananchi pamoja ndugu kuhusika katika kifo hicho kwani inadaiwa kuwa kijana Allen alidhoofika sana kwa kupigwa na kuteswa akiwa mikononi mwa Jeshi hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad