Jeshi la Polisi Mkoani Iringa Lafungua Jalada la Uchunguzi Juu ya Kutekwa kwa Abdul Nondo

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa Lafungua Jalada la Uchunguzi Juu ya Kutekwa kwa Abdul Nondo
Jeshi la Polisi mkoani Iringa limefungua kuwa jalada la uchunguzi kwa lengo la kufahamu ukweli juu ya Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo anaedaiwa kutekwa na watu wasiojullikana na kutelekezwa wilayani Mufindi.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amesema Nondo aliripoti kituo cha polisi cha Mafinga wilayani Mufindi.

“Baada ya kumhoji Nondo alisema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana ambao walimtekeleza Wilaya ni Mufindi,” -Kamanda Bwire

“Tunaendelea kufanya uchunguzi kama ametoa taarifa za uongo kwa nia ovu kwa lengo la kutaka kuhamasisha wanafunzi wenzake ili kuleta uvunjifu wa amani nchini tutamshughulikia kama wahalifu wengine na kama kweli atakuwa ametekwa tutawasaka wahalifu,” -Kamanda Bwire.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad