JIBU: Wanaouliza Uamuzi Gani Ungetolewa Mechi ya Simba vs Al Masry ingevunjika Kwa Giza au Mvua


Wakati mchezo wa kombe la shirikisho Afrika ukiendelea kati ya Simba dhidi ya Al Masry uwanja wa taifa, ghafla umeme ukakatika na kukawa na giza ambalo haliruhusu mchezo kuendelea na mvua kubwa ikaanza kunyesha. Mwamuzi wa mchezo huo Thando Helpus kutoka Afrika Kusini akasimamisha mchezo na timu zikarudi vyumbani.

Baada ya muda kupita baadhi ya taa za uwanjani zikawashwa ambapo mwanga ulitosha kuruhusu mchezo kuendelea na mvua iliyokuwa ikiendelea ikapungua. Wawakilishi wa timu zote mbili wakakutana na waamuzi na kukubaliana mechi iendelee ili kumalizia dakika zilizosalia.

Sasa maswali na mijadala imekuwa mingi kuhusu uamuzi ambao ungetolewa endapo umeme usingerudi au maji yangejaa uwanjani kiasi kwamba mechi isingeweza kuendea?

Mwenyekiti wa zamani wa Simba Ismail aden Rage amefafanua kanuni za mashindano hayo zinavyoelekeza nini cha kufanya endapo mechi inavunjika katika mazingira kama yaliyotokea wakati wa mchezo wa Simba dhidi ya Al Masry.

“Kwa kawaida katika mechi kama hizi za mashindano ya kombe la shirikisho kanuni zinasema kwamba, mwamuzi atasubiri kwa muda wa dakika 45 kama muda huo utakwisha umeme ukiwa haujarudi basi atavunja mechi na itarudiwa ndani ya saa 24 kama ni mchezo wa raundi ya kwanza ‘first leg match’ lakini ikiwa ni mchezo wa raundi ya pili ‘second leg’ taa zikazimika, atasubiri tena kwa dakika 45 lakini ikitokea umeme haujarudi, timu ngeni itapewa ushindi na timu mwenyeji itakuwa imeondolewa kwenye mashindano.”

“Sasa kuna watu wanajiuliza, wameona maji mengi uwanjani yaliyotokana na mvua kubwa lakini mwamuzi akaamua mchezo uendelee, tunarudi kwenye sheria 17 za mpira wa miguu, hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kuvunja mchezo au kuutambua uwanja unafaa au haufai kwa mechi isipokuwa mwamuzi peke yake.”

“Kwa hiyo mwamuzi aliona hali ya uwanja ina ridhisha ndio maana akaacha mechi iendelee.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad