Ikiwa zimesalia siku kadhaa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kufanya uchaguzi wa kumpata Rais wake mpya ambaye atarithi nafasi ya Rais wa sasa anayekaribia kumaliza muda wake Tundu Lissu baadhi ya wanaowania nafasi hiyo wameshaanza kampeni zao katika maeneo mbalimbali. Ikumbukwe kwamba kwa mujibu wa sheria uchaguzi wa TLS hufanyika kila baada ya mwaka mmoja.
Miongoni mwa wagombea hao leo tunaye Godfrey Wasonga ambaye aliita Waandishi wa habari ofisini kwake Dodoma na kuelezea mikakati yake endapo atapata nafasi hiyo.
Wasonga amesema …>>>”Nimekuwa na maono ya nafasi hii kwa muda mrefu sana na naamini huu ndio wakati muafaka, endapo nitachaguliwa kwanza nitahakikisha tunaiomba Serikali ibadilishe sheria ili uchaguzi huu uwe unafanyika kila baada ya miaka mitatu na sio mwaka mmoja kama ilivyo sasa”- Godfrey Wasonga
“Kwa kuanzia nikipata nafasi hii nitatoa ardhi ya heka kumi katika eneo lililo karibu na inapojengwa Ikulu ya nchi kwa ajili ya sisi kujenga makao makuu ya chama chetu cha TLS na nitashawishi baadhi ya watumishi kuhamia Dodoma” – Godfrey Wasonga